8  Mpangilio wa maneno

8.7 Nafasi ya kielezi kwenye fungu la maneno

Kielezi halisi huja baada ya somo kamili (x) na somo la taarifa (o) kwenye fungu kuu la maneno.

Jeg besøgte ikke min søster i går.
x o          

Sikumtembelea dada yangu jana.
x o      

Han kommer måske i morgen.
x o    

Labda atakuja kesho.
  x o  

Kwenye fungu la maneno na mpangilio wa maneno kwa kupindua huja kielezi kwanza baada ya somo la taarifa (o) na somo kamili (x).

Kommer han måske i morgen?  
o x      

Atakuja kesho labda?
x o    

Kama mtu anatia  mkazo maana kamili ya kielezi, kielezi huwekwa kwanza kwenye fungu la maneno.

Måske kommer han i morgen.
  o x  

Labda atakuja kesho.
  x o  

Ulinganisho:
Kwa kiswahili  kielezi kinaweza  kuwa mwanzoni mwa fungu la maneno, lakini ni mpangilio wa maneno wa moja kwa moja pia kwenye fungu la maneno.

Kielezi kila wakati husimama katikati ya somo kamili (x) na somo la taarifa (o) kwenye fungu nusu la maneno.  

Lone sagde, at hun ikke havde travlt.
      x   o  

Lone alisema, kwamba hakuwa kazi nyingi.
      x o    

Kwenye somo la taarifa ambalo limechanganyika (kwa mfano: alitumia, alitembelea, aliona) lazima kielezi kiwe katikati ya maneno mawili kwenye somo la taarifa.

Jeg har ikke besøgt min søster.
x o1   o2    

Sikumtembelea dada yangu.
x o  

De har ofte set hinanden.
x o1   o2  

Walionana mara nyingi.
x o  

Kielezi  huja mwisho kwenye fungu la maneno, kama kitu halisi   (∆) ni badala ya jina la mtu (-angu, -ake, -etu n.k).

Bila badala ya jina:

Hr. Hansen kører altid sin bil.
x o  

Bwana Hansen anaendesha gari yake siku zote.
x o
   

Pamoja na badala ya jina:

Hr. Hansen kører den altid.
x o  

Bwana Hansen analiendesha siku zote
x ∆ o  

Bila badala ya jina:

Jeg ser ikke Søren.
x o  

Simuoni Søren.
   

Pamoja na badala ya jina:

Jeg ser ham ikke.
x o  

Simuoni.
 

Kama kuna vielezi zaidi kwenye fungu la maneno, vielezi hivyo hufuatana.

Lis har jo altid bagt kage.
x o1     o2  

Lis siku zote alipika keki.
x   o1 o2  

Ulinganisho:
Kwa kiswahili neno la kukana ikke linakuwa ni silabi kwenye tendo. Silabi hiyo inabadilika kutegemeana na watu tofauti. Kama ikke haikai yenyewe kwenye tendo, silabi husimama yenyewe kama neno.

Maneno mengine huweza kukaa mwanzoni, katikati, na mwishoni kwenye fungu la maneno bila fungu hilo kubadilisha maana.

Simuoni.
Humuoni.
Sikumuona.
Hukumuona.

Maswali ya ufahamu