8  Mpangilio wa maneno

8.2 Upinduaji wa mpangilio wa maneno

Zaidi ya mpangilio wa maneno wa moja kwa moja kunakuwa na upinduaji wa mpangilio wa maneno. Kwenye fungu la maneno ambako kuna upinduaji wa mpangilio wa maneno huja somo la taarifa (o) kabla ya somo kamili (x).

Kuna upinduaji wa mpangilio wa maneno katika swali, na kama fungu la maneno linaanza na somo lingine zaidi ya somo kamili kwa mfano wakati au mahali maalum (ang. 8.4, 8.5, 8.7).

Maswali:

Sover manden?   Mwanamume amelala?
o x   x o

Spiser han?   Anakula?
o x   xo

Ulinganisho:
Kwa kiswahili hakuna upinduaji wa mpangilio wa maneno kwenye maswali. Swali hufanyika kwa kupandisha sauti juu.

Wakati kwenye mpangilio wa maneno wa moja kwa moja:

Jeg besøgte min tante i går.   Nilimtembelea shangazi yangu jana.
x o         x o    

kwa upinduaji wa mpangilio wa maneno:

I går besøgte jeg min tante.   Jana nilimtembelea shangazi yangu.
    o x     o x  

Mahali kwenye mpangilio wa maneno wa moja kwa moja:

Jens bor i Sverige.   Jens anaishi Sweden.
x o       x o  

kwa upinduaji wa mpangilio wa maneno:

I Sverige bor Jens.   Jens anaishi Sweden.
    o x   x o  

Wakati wa kutumia majina ya kuuliza, jina la kuuliza kila wakati linakuja mwanzoni mwa fungu la maneno, na somo la taarifa (o) linakuja baadaye.

Majina ya kuuliza ni: hvem, hvad, hvor, hvornår, hvilken/hvilket/hvilke, hvor længe, hvordan, hvorfor, hvis.

Hanne bor i København.   Hanne anaishi København.
x o       x o

 


Hvor bor Hanne?   Hanne  anaishi wapi?
  o x   x o  

Peter spiser kage.   Peter anakula keki.
x o   x o

Hvem spiser kage?   Nani anakula

keki?

x o   x o

Peter spiser kage.   Peter anakula keki.
x o   x o

Hvad spiser Peter?   Peter anakula nini?
o x   x o

Kwenye upinduaji wa mpangilio wa maneno, ambako kuna matendo mawili kwenye fungu la maneno, somo kamili lazima lisimame katikati ya matendo hayo mawili.

torsdag skal jeg rejse til København.
    o1 x o2    

Alhamisi ni lazima nisafiri kwenda København.
  o1 x o2    

Ulinganisho:
Kwa kiswahili hakuna upinduaji  wa mpangilio wa maneno hata kama wakati au mahali huja kwanza kwenye fungu la maneno.

Maswali ya ufahamu