Kama fungu la maneno liko kwa wakati uliopita, na kitendo kimetokea mara moja tu hutumika da. Kama kitendo kinatokea mara nyingi hutumika når.
Jeg købte en bil, da jeg var i Silkeborg. | Nilinunua gari wakati nilipokuwa Silkeborg. |
Vi spiste altid kartofler, når vi besøgte min mor. | Tulikula viazi siku zote wakati tulipomtembelea mama yangu. |
Når hutumika pia kwenye wakati uliopo na wakati ujao.
Han går i seng, når han er søvnig. | Anakwenda kitandani wakati anaposinzia. |
Jeg skal købe en jakke, når jeg får penge. | Nitanunua koti wakati nitakapopata pesa. |
Ulinganisho:
Kwa kiswahili hakuna tofauti kati ya når na da. Hutumika neno moja tu wakati.