7  Maneno ya kuunga

7.2 Mpango wa maneno ya kuunga kwa kutolingana

Mpango wa maneno ya kuunga kwa kutolingana, huunganisha mafungu mawili ya maneno. Kila mara huzungumzia kuhusu fungu kuu la maneno na fungu nusu la maneno.
Mpango wa maneno ya kuunga kwa kutolingana wakati wote huanzia na fungu nusu la maneno (ang. 8.3 Mpangilio wa maneno kwenye fungu la maneno).

Mens jeg kørte, regnede det.

Wakati niliendesha mvua ilinyesha.

Hun spurgte, om jeg elskede hende.

Aliniuliza kama nilimpenda.

Mpango wa maneno ya kuunga kwa kutolingana ni: at, da, dengang, end, for at, efter at, fordi, før, førend, hvis, idet, inden, medmindre, mens, når, om, selvom, siden, skønt, som, som om, så at, uden at.

Hun spørger, om vi kommer i morgen.

Anauliza kama tutakuja kesho.

Han kommer, når han får tid.

Atakuja wakati akipata nafasi.

Vi gik tidligt, fordi vi var færdige.

Tulikwenda mapema kwa sababu tulikuwa tumemaliza.

Ulinganisho:
Kwa kiswahili mpango wa maneno ya kuunganisha kwa kutolingana hutumika sawa kama kwa kidenish.

Maswali ya ufahamu