7  Maneno ya kuunga

7.1 Mpango wa maneno ya kuunga kwa kulingana

Mpango wa maneno ya kuunga kwa kulingana huunganisha maneno, masomo, na mafungu ya maneno ya aina moja. Kwa mfano majina kwa majina, sifa kwa sifa, au fungu kuu la maneno kwa fungu lingine kuu la maneno.

Mpango wa maneneo ya kuunga kwa kulingana ni: og, men, eller.

Manden og konen kører sammen.

Mume na mke wanaendesha pamoja.

   

Kaffen er stærk, men dejlig.

Kahawa ni kali lakini ni nzuri.

   

Kommer du hjem i eftermiddag, eller kommer du først i aften?

Utakuja nyumbani machana, au utakuja jioni.

Ulinganisho:
Kwa kiswahili mpango wa maneno ya kuunga kwa kulingana hutumika sawa kama kwa kidenish.

Maswali ya ufahamu