5  KIelezi

5.0 Ubainisho

Kielezi huzungumzia kuhusu jinsi kitu kinavyotokea. Kielezi kinaweza pia kuelezea kamili zaidi hvor (wapi), hvordan (vipi), hvornår (lini) hali, mwendo, au mabadiliko yanayotokea.

Børnene kom ind.

Watoto walikuja ndani.

Han sang dårligt.

Aliimba vibaya.

Børnene vågnede tidligt om morgenen.

Watoto waliamka mapema asubuhi.

Kielezi huelezea matendo na siyo vitu kama maneno ya sifa.

Kielezi kinaweza kukaa pamoja na tendo, sifa, kielezi kingine au fungu zima la maneno.

Solen gik ned.

Jua lilikuchwa.

Bilen er ikke ny.

Gari siyo mpya.

Jeg ser ham næsten aldrig.

Simwoni karibu hata mara moja.

Han kommer måske en halv time for sent.

Labda atakuja amechelewa nusu saa.

Kielezi hugawanyika kwenye halisi na bandia.

Maswali ya ufahamu