4  Sifa

4.2 Ngazi za sifa

Sifa nyingi zaidi zinakuwa na ngazi. Ina maana kwamba neno sifa huelezea ngazi tofauti ambazo huweza kulinganishwa.

Danmark er et koldt land.

Danmark ni nchi ya baridi.

Norge er koldere end Danmark.

Norwey ni baridi zaidi kuliko Danmark.

Grønland er koldest.

Greenland ni baridi sana.

Sifa huongezea -ere au -re kwenye ngazi ya juu na -est au -st kwenye ngaziya juu zaidi.

Ngazi za sifa

Neno halisi

Ngazi ya juu

Ngazi ya juu zaidi

kold

koldere

koldest

pæn

pænere

pænest

varm

varmere

varmest

Sifa ambazo zina silabi nyingi, au ambazo aina za sifa (ang.1.5 Kabla ya wakati uliopo) kutoka tendo, ngazi zake mara nyingi hazina nyongeza mwishoni, lakini kuna kuwa na mere na mest mwanzoni mwa aina ya neno halisi.

jeg er sulten Nina njaa
Han er mere sulten end mig. Ana njaa zaidi yangu.
Hun er mest sulten. Ana njaa sana.
Jeg er interesseret i popmusik. Ninapendelea muziki wa pop.
Hun er mere interesseret i rockmusik. Anapendelea zaidi muziki wa rock.
De er mest interesseret i klassisk musik.

Wanapendelea sana muiki wa klasiki.


Ngazi za sifa

Neno halisi

Ngazi ya juu

Ngazi ya juu zaidi

fremmed

mere fremmed

mest fremmed

interesseret

mere interesseret

mest interesseret

Ulinganisho:
Kwa kiswahili ngazi za sifa kwenye ngazi ya juu, hutumika sana baada ya sifa na kwenye ngazi ya juu zaidi hutumika zaidi.

Maswali ya ufahamu