3  Badala ya jina

3.6 Marejeo ya badala ya jina

Marejeo ya badala ya jina ni jina ambalo huelezea nyuma kwa jina ambalo lilikuwa kabla au somo. Badala ya jina mengi ya kawaida ni som na der.

Pigen, som hedder Susanne, bor i Nygade.

Msichana ambaye anaitwa Susanne, anaishi Nygade.

Pigen, der hedder Susnne, bor i Nygade.

Msichana ambaye anaitwa Susanne, anaishi Nygade.

Som na der inaonyesha nyuma pigen. Wakati som na der ni somo kamili, ni sawa sawa tu kama kwa kutumia som au der. Kama marejeo ya badala ya jina nikitu halisi, ni lazima kutumia som.

Han spiste maden, som jeg gav ham.

Alikula chakula ambacho nilimpa.

Ulinganisho:
Kwa kiswahili marejeo ya badala ya jina hutegemeana na neno amabalo linaonyeshwa. Kwa hiyo hutegemeana na aina gani ya zile aina saba za majina, na kama ni umoja au ni kwa wingi.

Chumba ambacho tulipanga.
Vyumba ambavyo tulipanga.
Mtoto ambaye anacheza.
Watoto ambao wanacheza.

Maswali ya ufahamu