3  Badala ya jina

3.3 Jamaa ya badala ya jina la kumiliki

Jamaa ya badala ya jina la kumiliki hutumika badala ya hans, hendes, dens na dets, wakati wa kuzungumzia kitu chake kwa mtu 3. Hapa kuna tofauti pia katika neno n- na neno t-.

neno -n: sin

neno -t: sit

wingi
: sine

en kjole  
Hun skal vaske sin kjole. Ni lazima afue gauni lake.
   
et hus                
Hun maler sit hus. Anapiga rangi nyumba yake.
   
bøger  
Lars har læst alle sine bøger. Lars amesoma vitabu vyake vyote.

Ulinganisho:
Kwa kiswahili hakuna mgawanyo kati ya kitu chake kwenye mtu wa 3. umoja, na vitu vya mtu mwingine.

Maswali ya ufahamu