2  Majina

2.4 Mwisho kwenye wingi

Mwisho kwenye wingi kuna aina mbili tofauti.

Kama jina lina silabi moja kawaida linaishia na -e kwenye aina ya isiyodhahiri na -ene kwenye aina ya dhahiri.

Kama jina lina silabi mbili au zaidi, jina linaishia na -er kwenye aina ya isiyodhahiri na -erne kwenye aina a dhahiri.

Majina kwenye wingi

Isiyodhahiri

Dhahiri

aviser

aviserne

haver

haverne

huse

husene

drenge

drengene

Ulinganisho:
Kwa kiswahili kuna aina saba za majina. Aina hizi za majina herufi za mwanzo hubadilika kwenye wingi kutegemeana na ni aina gani ya majina inayozungumziwa.

mtoto - watoto
kiti - viti
mti - miti

Maswali ya ufahamu