Kwenye umoja kuna aina mbili: isiyodhahiri na dhahiri.
Kwenye isiyodhahiri majina hayajulikani.
En dreng larmer altid. |
Mvulana anapiga kelele kila wakati. |
Et hus bliver repareret. |
Nyumba inatengenezwa. |
Kwenye dhahiri majina yanajulikana.
Drengen larmer altid. |
Mvulana anapiga kelele kila wakati. |
Huset bliver repareret. |
Nyumba inatengenezwa. |
Neno n- kwenye aina ya dhahiri, huishia na -en.
Lakini kama jina linaishia na -e, mwisho ni -n tu.
Neno t- kwenye aina ya dhahiri huishia na -et.
Lakini kama jina linaishia na -e, mwisho i -t tu.
Majina kwenye umoja |
|
---|---|
Isiyodhahiri | Dhahiri |
en avis | avisen |
en have | haven |
et hus | huset |
et værelse | værelset |
Ulinganisho:
Kwa kiswahili hakuna dhahiri na isiyodhahiri.