1  Tendo

1.7 Aina ya -w-

Matendo yote yako mara nyingi zaidi kwenye aina ya ku-. Aina ya ku- ina maana kwamba ni somo kamili ambalo linafanya hicho ambacho tendo linaelezea.

Pigen spiser maden. Msichana anakula chakula.

Pigen ni somo kamili na spiser ni tendo halisi kwenye aina ya ku‑. Tendo hupatikana pia kwenye aina ya -w-. Aina ya -w- ina maana kwamba somo kamili halifanyi kitu lakini linafanyiwa kitu.

Maden spises af pigen.

Chakula kinaliwa na msichana.

Maden ni somo na spises ni tendo kwenye aina ya -w- na af pigen ni muungano wa maneno ya hali. Maden ni somo kamili lakini siyo aina ya ku-.

Aina ya -w- hufanyika kwa aina mbili. Ama kwa kuishia na -s kwenye tendo au kwa at blive na aina fupi ya sifa.

Aina ya -w- inayoishia na -s hutumika wakati kitu cha kawaida kinapotokea au kitu kinapotokea mara kwa mara. Aina hii huelezea kazi fulani. Kama ni wakati uliopo, aina ya tendo huishia na -s. Kama ni wakati uliopita, mwishoni huongezea -s kwenye aina ya wakati uliopita.

Grønsagerne koges i 15 min.

Mboga zinachemshwa kwa dakika 15.

Stoffet sys sammen i siderne.

Kitambaa kimeshonwa pamoja pembeni.

Postkassen tømtes kl. 9.

Sanduku la posta linakuwa tupu saa 9.

Aina ya -w- pamoja na aina ya at blive na aina fupi ya sifa (ang. 1.5 Kabla ya wakati uliopo) hutumika wakati wa kuelezea kuhusu kitendo ambacho hutokea mara moja tu. Katika mazungumzo mara nyingi hutumika blev, wakati ambao ni wakati uliopita na siyo -s, hata kama huzungumzia kuhusu kitendo ambacho kinatokea mara nyingi.

Maden bliver spist af pigen.

Chakula kinaliwa na msichana.

Maden blev spist af pigen.

Chakula kililiwa na msichana.

Ulinganisho:
Kwa kiswahili -a huondoka kutoka kwenye tendo halisi na mwisho mpya -wa huongezewa.

kula          - kuliwa
kushona    - kushonwa

Maswali ya ufahamu