1  Tendo

1.6 Wakati ujao

Wakati ujao huelezea kuhusu kitu ambacho kitatokea wakati unaokuja. Wakati ujao hufanyika kwa vil au skal pamoja na aina ya kitendo au kwa wakati uliopo pamoja na ishara ya wakati.

Jeg vil rejse til Amerika.

Nitasafiri kwenda Amerika.

Jeg skal spise.

Nitakula.

Jeg rejser til Amerika i morgen.

Nitasafiri kwenda Amerika kesho.

Ulinganisho:
Kwa kiswahili wakati ujao huongezea ta- mwanzoni mwa tendo halisi. Kabla ya ta- huanzia na ni, u, n.k. kutegemeana na watu tofauti.

Nitakula.                                            
Utakula.

Maswali ya ufahamu