1  Tendo

1.4 Wakati uliopita

Wakati uliopita huelezea kitu ambacho kilitokea kabla kwenye wakati maalum.

Hun vaskede tøj.

Alifua nguo.

Pigen spiste maden.

Msichana alikula chakula.

Kuna aina mbili za taratibu zinazoonyesha kwenye wakati uliopita. Aina ya kwanza ni tendo halisi linaloishia na -ede. Nyingine ni tendo halisi linaloishia na -te.

Wakati uliopo kuishia na -ede

Tendo halisi

Wakati uliopo

Wakati uliopita

lav

laver

lavede

bo

bor

boede

vask

vasker

vaskede


Wakati uliopo kuishia na -te

Tendo halisi

Wakati uliopo

Wakati uliopita

køb

køber

købte

spis

spiser

spiste

lås

låser

låste

Jambo la pekee: Tendo ambalo siyo la kawaida linaweza kuunganishwa kwa aina nyingi tofauti. Kuna matendo karibia 150 ambayo siyo ya kawida.

Matendo yasiyo ya kawaida

Tendo halisi

Wakati uliopo

Wakati uliopita

går

gik

stjæl

stjæler

stjal

se

ser

Ulinganisho:
Kwa kiswahili huongeza li- kwenye tendo halisi. Kabla ya li- tendo halisi huanza na: ni, u, n.k. kutegemeana na watu tofauti.

Nilikula.
Ulikula.


Maswali ya ufahamu