1  Tendo

1.3 Wakati uliopo

Wakati uliopo huelezea kitu ambacho kinatokea sasa hivi au hutokea zaidi mara nyingi.

Jeg går nu.

Ninakwenda sasa.

Barnet sover godt.

Mtoto analala vizuri.

Wakati uliopo ni muungano wa tendo halisi ambalo huishia na ­­‑er katika tendo lenyewe. Kama aina ya kitendo haiishii na -e huishia na-r.

Tendo katika aina ya kitendo wakati uliopo

Namna ya tendo

Tendo halisi

Wakati uliopo

at spise

spis

spiser

at køre

kør

kører

at lave

lav

laver

at gå

går

Ulinganisho:
Kwa kiswahili wakati uliopo huanza na herufi na- kwenye tendo halisi. Kabla ya na- huanzia na ni, u, n.k. ambayo huelezea ni mtu gani anayezungumziwa.

Ninakula.
Unakula.

Maswali ya ufahamu