Tendo huelezea kitendo au hali. Ina maana, tendo husimulia habari ya hali, kwamba unafanya kitu au kitu kinafanyika.
Hun sover. |
Analala. |
Pigen spiser mad. |
Msichana anakula chakula. |
Bilen kører hurtigt. |
Gari inakwenda mbio. |
Koppen står på bordet. |
Kikombe kiko juu ya meza. |
Kwa kidenish tendo halibadiliki kwenye herufi za mwisho kwa watu tofauti. Tendo hubadilika kwenye herufi za mwisho katika nyakati tofauti, lakini huitwa sawa sawa kwa watu wote kwenye wakati tofauti.
Muungano wa tendo kwa watu tofauti |
||
Mtu |
Wakati uliopo umoja |
Wakati uliopo wingi |
Mtu 1. |
Jeg spiser |
vi spiser |
Mtu 2. |
Du spiser |
I spiser |
Mtu 3. |
han/hun/den/det spiser |
de spiser |
Ulinganisho:
Kwa kiswahili tendo hubadilika kutegemeana na wakati na watu tofauti.